Bongo Tube Blog

BongoTube Tanzania Videos

TANZANIA VIDEOS. News, Celebrities, Music, Sports, Tourism, Comedy, Recipes...

For any question or request e-mail us bongotube11@gmail.com

News - Habari

Important Notice: The BongoTube Blog is a free and apolitical blog wich does not support any political party in Tanzania. So, we post videos talking about any political party like wich is governing and any other in the opposition, as a symbol of FREEDOM OF EXPRESSION





Mwigulu ni Mzushi

by CHADEMA tv


Katibu Mwenezi wa Kata ya Saranga Bw. Perfect Mwasiwelwa ameibuka na kukanusha taarifa aliyoitoa Naibu Katibu Mkuu wa CCM Taifa Mwigulu Nchemba kuwa yeye amehamia CCM. Bw.Perfect amesema aliyejitambulisha Jukwaani si yeye na inaelekea amepandikizwa kwa maslahi ya Mwigulu mwenyewe.








Watu 4 wajeruhiwa, magari 24 yaharibiwa kituo cha mabasi Ubungo...

by ITV TANZANIA


Watu wanne wamejeruhiwa,huku magari madogo zaidi ya 24 ya watu binafsi yakiharibiwa vibaya katika kituo cha mabasi yaendayo mikoani na nchi za jirani cha Ubungo jijini Dar-es-salam baada ya kuangukiwa na ukuta.







RAY C ALIPOKWENDA KUMSHUKURU RAIS KIKWETE IKULU

by ITV TANZANIA


Siku mwanamuziki wa Kizazi Kipya Rehema Chalamila, maarufu kama RAY C, alipomtembela Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete Desemba 10, 2012 Ikulu jijini Dare s Salaam na kumshukuru kwa msaada wa matibabu aliyompatia wakati alipokuwa mgonjwa hivi karibuni. Rehema aliyefuatana na Mama yake Mzazi Margareth Mtweve na Dada yake Sarah Mtweve alimweleza Rais kuwa afya yake sasa imeimarika na kwamba muda si mrefu ujao atarejea jukwaani kukonga nyoyo za mashabiki wake. Kwa upande wake, Mama Mzazi wa Ray C amemshukuru Rais Kikwete kwa kuokoa maisha ya mwanaye na vilevile ametoa wito kwa watu wanaokusanya michango kwa ajili ya mwanaye waache kufanya hivyo kwani matibabu ya Ray C yamegharamiwa na Rais.








Kamati ya Troika yakutana jijini Dar es Salaam.

by ITV TANZANIA


Kamati ya siasa ulinzi na usalama ya maendeleo ya nchi za kusini mwa Afrika- Troika imeendelea na msimamo wa kumtaka rais wa serikali ya mpito ya Madagasca Bwana Andry Rajolina kutogombea katika uchaguzi mkuu huku kiongozi huyo akiomba kujadiliana na wenzake.









The Ruling Party should Stop using Police for Political issues in Tanzania

by chadematv


In Tanzania Politics it have been normal trend for the rulling Party CCM to use the Police force to oppress the Opposition Parties since the multiparty system started in Tanzanzia. Due to that many people have been killed and a lot of them be injured, arrested and prisoned. The latest trategy is the killing of Mr.Daud Mwangosi the Journalist with Chanel Ten TV Station in Tanzania while he was covering the meeting of CHADEMA at Nyololo District in Iringa region in Tanzania. It now the time for International Community to intervin so as to save the life of innocent citizen and the growth of free democracy in Tanzania.








Tanzania yatupilia mbali ombi la kuuza pembe za ndovu

by Standard Group Kenya


Serikali ya Tanzania imetupilia mbali ombi lake la kutaka ruhusa ya kuuza pembe za ndovu na bidhaa zake kwenye mkutano ujao wa 'cites' utakaoandaliwa mwezi machi, mjini bangok, thailand. Ombi la tanzania lilikuwa limeleta hali ya mshike mshike kati ya serikali za Kenya na Rwanda ambazo zinapinga kuuzwa kwa pembe za ndovu pamoja na bidhaa zake, na huenda ingalihujumu uhusiano wa mataifa hayo jirani na Tanzania kwenye harakati za kuhifadhi ndovu
Watch KTN Streaming LIVE from Kenya 24/7 on http://www.ktnkenya.tv

No hay comentarios:

Publicar un comentario